
Misukosuko,uhasama na chuki inyoshuhudiwa katika muungano wa chama cha jubilee sio kitu ambacho hakikutarajiwa hasa ikizingatiwa ubinafsi wa mtu,kabila na kundi la watu Fulani waliokuwa wakishikilia mwaka wa uchaguzi unavyokaribia.
Ni mienendo ambayo imeshuhudiwa kila mara uchaguzi mkuu unavyonukia nchini Kenya na yanayomkumba naibu wa rais William Ruto sio tofauti kwa sasa.
Mchanganuzi wa maswala ya kisiasa Erick Onsongo ambaye pia ni mahdhiri katika chuo kikuu cha kisii anahoji kuwa kuna mawimbi ya kundi Fulani katika chama tawala cha jubilee ambao huenda hawajakuwa na uhusiano mwema na ruto kutoka awali wanaotaka kutumia mbinu ya kuubadilisha uongozi wa chama.
Kwa upande mwingine Onsongo anadai kuwa pia kuna uwezekano wa wasawishi na mababe wa ufadhili wake uhuru Kenyatta kuwa rais wanaotikisika na mhemko wa Ruto kambini kwa sababu walichokitaka ni uongozi ambao wako nao na hawaoni tena umuhimu wake kambini na hivyo afurushwe.
“Siasa za Kenya zimejaa ubinafsi,tama,hila na wivu wa hali ya juu kwamba kinachoendelea aitha alivyosema tuju ni agizo la rais kama mwenyekiti wa chama,kundi Fulani la wanasiasa ambao siasa zao ni kugonganisha watu kwa misingi ya wivu kama david murathe na maina kamanda,alafu kuna mbinu fiche ya kumnufaisha ruto kwa kuwa kila wakati ameonekana kama anayeonewa hasa kutoka kwa kabila ambalo aliliunga mkono kuutwaa uongozi”,akamaka Onsongo.
Kulingana naye kwa sasa ni furaha kwa jamii ya odm na haswa kiranja wake Raila Odinga kwani amefanikiwa kuwasha moto ambao kuuzima ni kama alichokitendea chama cha kanu wakati marehemu mzee moi alimfanya katibu mkuu wa chama na akakivunjilia mbali.
Mtafaruku huu huenda ukasababisha mengi hasa kati ya pande mbili zilizopo ndani ya jubilee kama kieleweke kundi linalomuunga mkono rais Uhuru Kenyatta na muungano wake na raila odinga na kundi linguine la tangatanga linalomuunga mkono William ruto.
Huku kundi la tangatanga likiona msukumo wa barua ya Raphael Tuju kama msawasha wa kuja pamoja kwa Raila na uhuru ili kuuwa ndoto yake kuwa rais 2022,wale wa kieleweke wanashikilia dhana kuwa hamna deni la kulipa analo uhuru kwa ruto na kwamba jubilee haipo tena ila wanatafuta miungano ya kuhakikisha wapo serikalini 2022.
Kulingana na mbunge wa mugirango kusini Silvanus Osoro kwa siasa kuna usaliti na hujuma ambayo hufanywa namagenge Fulani ya vyama na miungano ya kisiasa ili wapambane visawasawa kwenye ulingo wa siasa majaribu ambayo kulingana naye naibu wa rais ashapitia kwani amekuwa siasani kwa mda mrefu kwa kujipigania wala sio kubebwa.
“Ukiangalia vizuri naibu wa rais amejipigania kisasa kutoka awe mbunge wa turbo hadi sasa ni naibu wa rais wengi msingi wa siasa zao ni jamii na ukoo vitu ambavyo havidumu kwa mda mrefu kwa sababu pia wakenya wamegutuka na yakini mafikirio yao kwa sasa yamepigwa na mwangaza”,anasema Osoro huku akionya kuwa mwanasiasa yeyote huwa amejipanga kwa matukio yoyote walakin wao kama wanaomuunga mkono Ruto watatumia akili zao vikamilifu.
Osoro anasisitiza kuwa kuna mengi ambayo yanadhihirisha kuwa ukabila umerudia hali yao ya awali kwani ukitamzama David Murathe,Maina Kamanda,Ann Waiguru na wengine na matamshi wamekuwa wakitoa kuhusu wakikuyu na kumuunga mkono Ruto kuwa rais 2022 kuna swala ambalo sisi kama wakenya tunafaa kutafakari kuhusu ni nani anamcheza mwenzake kisiasa kuhusiana na uongozi.
“Haiwezi kuwa eti ni watu wa jamii Fulani pekee ndio wanaona eti naibu wa rais ni mbaya ilhali hawakuyaona hayo alipotoa msaada wa kura kwa ushindi uliopo huu ni unafiki wa kiwango cha hali ya juu na kulingana na mimi msimu huu mabepari wa kisiasa wamejianika uwanjani wapiga kura kuwaona na kuamua”,akarudia Osoro akiongeza kuwa sarakasi za kisiasa zinzofanywa na tuju na kundi lake ni hekaya za abunuasi na kwamba inahuzunisha kuwa badala ya viongozi wengine kuunga mkono vita dhidi ya corona siasa zipo vichwani mwao kila saa.