Utawala wa Mkoa walaumiwa kufuatia ongezeko la visa vya unajisi Kisii

0
318
Picha/Kwa hisani
Picha/Kwa hisani

Utata umezuka baada ya madai kuibuka kuwa msaidizi wa chifu mmoja kutoka gucha kusini kaunti ya kisii ameficha matokeo ya uchunguzi uliofanywa kuhusu madai ya kubakwa kwa mwanafunzi mmoja msichana mwenye umri wa miaka 13 kutoka shule moja ya kibinafsi.

Chifu huyo ambaye ametambulika kama Brian Oteyo anadaiwa kukifanya kitendo hicho mbele ya vijana wake wa mkono katika afisi yake ilioko eneo la gotichaki lokesheni ndogo ya nyansore  hamna ripoti ambayo iliandikishwa katika kituo chochote cha polisi wala katika ndani ya chifu huyu.

Inadaiwa kuwa vijana hao wa mkono wa chifu huyo walifahamishwa kuwa kuna wavulana watatu ambao wanafinyanga matofali katika eneo hilo na ambao walionekana wakimvuruta mwanafunzi huyo msichana kwenda mahala wanakoishi mapema na asubuhi.

Kulingana na mwanafunzi ambaye jina lake litabanwa kwa sasa ni kwamba alipokuwa akienda shule ya kibinafsi ambayo ipo karibu na mahali wanakoishi alishtukia wavulana watatu ambao anawajua wakamvuruta kasha akapiga nduru ili angaa apate msaada walakin badala ya kupokea haki alinyanyaswa kwa kupigwa viboko.

‘’Nilipopiga nduru huku wakinivuruta kuna wasaidizi wa chifu walikuwa wakipita wakagonga mlango na walikuwa washanifanyia madhambi mabaya ,nikitarajia kupewa msaada sasa mimi ndio nilienda na washukiwa kasha tukakalishwa chini mchana wote na mamangu alipokosa hela za kuwasafirisha hadi kwa kituo cha polisi wakaachiliwa”,akasimulia msichana huyo aliyedai kuwa alipitia wakati mgumu kuelewa ni kwa nini alikuwa anatolewa damu kwa kidole badala ya yeye kufanyiwa uchunguzi na ripoti kuandikwa.

Kufika katika eneo la mkasa waliwashika wavulana hao na mwanafunzi huyo kasha wakawapeleka hadi afisi ya chifu ilioko kilomita tatu kutoka eneo la mkasa kabla hata ya ufahamu kuwaendea wasimamizi wake kama wazazi.

Kulingana na mamake mtoto huyo Judith jemima okong’o,alipigiwa simu aende kwa afisi ya chifu ghafla na alipofika huko akapata washukiwa wavulana hao watatu na mwanawe msichana ambaye alidhulumiwa wamekalishwa chini,chifu akamuamuru mamake msichana atafute shilingi elfu mbili za kuwasafirisha mahabusu wake hadi kituo cha polisi cha nyamarambe.

“Ndio niliamrishwa na chifu kutafuta piki piki[bodaboda]niwasafirishe mahabusu wangu hadi nyamarambe ambao ni wavulana hao watatu,nikakosa elfu mbili mimi na mia tano yangu nikaita waendeshaji wa pikipiki kufika kwa chifu walakini aliwafukuza kasha akawaachilia washukiwa na kunipatia msichana wangu nikaenda naye”,alisimulia mama huyo akidai kuwa usiku wa manane usiku huo chifu tena akaja eti anataka kumpeleka motto wangu hospitalini nyamarambe.

Mama huyo anaeleza kuwa yeye pamoja na babake walilazimika kungoja kwa foleni huku chifu akikazana na motto kumpeleka kutoka jumba moja hadi linguine bila kuwajulisha.

Walitoka hospitalini nyamarambe bila ya matokeo yoyote huku chifu akiwaambia kuwa msichana hakubakwa ilivyodaiwa jambo ambalo liliwatia wasiwasi na kutia doa kilichokuwa kikiendelea wakati chifu alikuwa akipitapita ndani ya hospitali hiyo.

Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya gucha kusini Edonga Nanok  alikana kuwa na ufahamu kuhusu madai hayo kisha akashauri kuwa ombi rasmi la uchunguzi iandikwe chini na ikabidhiwe ofisi ya ili uchunguzi uanzishwe kuhusu madai hayo.

Naibu chifu huyo hakupokea simu zetu wala kujibu jumbe fupi tulizokuwa tukimwandikia,mama mzazi anaomba serikali imfanyie haki yeye hasa kwa kupata matokeo ya uchunguzi wa kilichomfanyikia mwanawe kutoka kwa hospitali ya nyamarambe.

Washukiwa hao kulinga na wanakijiji wamekuwa na mazoea hayo ya kuwabaka wasichana kwa kuwavuruta kwenda kwa nyumba yao na afisi ya chifu huyo imekuwa ikipokea malamishi hayo bila kufanya chochote .