
Uhasama kati ya gavana wa kaunti ya kisii James Ongwae na naibu wake Joash Maangi unaendelea kuchacha.
Katika hatua za hivi karibuni kabla ya mchakato wa BBI na mkutano uliofanyika ndani ya uga wa Gusii stadium tarehe kumi Januari na ambao uliwaleta viongozi wa matabaka mbalimbali pamoja na kuongozwa na kinara wa ODM Raila Odinga,Maangi alionekana kuupinga mkutano huo.
Akizungumza katika makao yake rasmi naibu huyo wa gavana aliutupilia mbali mkutano huo akisema kuwa haukuwa wa manufaa yoyote kwa mwananchi wa kawaida kwa sababu watu wote wa eneo hili hawakuwa na upinzani wowote na BBI.
Maangi alisema kuwa mkutano huo ulilenga kueneza siasa na kutumia mali ya serikali pia kaunti vibaya.
”wacha niseme papa hapa na leo kwamba kila mtu amekaribishwa kwa mkutano lakini ieeleweke kwamba kuna mahitaji mengi ambao tungepatiana kwa mtizamo wa kwanza kuliko kuleta BBI ilhali hamna mwenye anaipinga”,alisema naibu huyo gavana.
Aliungwa mkono na wawakilishi wa wadi wapatao ishirini,wakiongozwa na mwakilishi wa wadi ya kiogoro Samwel Apoko wote kwa pamoja walitaka miswada ambayo huwa wanapitisha katika bunge la Kisii haioni mwanga wa siku hasa kwa kupatiwa sikio la kufa na usimamizi mkuu.
Mgogoro huwa haukusitisha wala kusababisha hitlafu yoyote kwa mpangilio wa mkutano huo ambao ulifanikiwa kutekelezwa huku ukiungwa mkono na wengi wa watu waliohudhuria akiwemo aliyekuwa waziri mkuu na kinara wa ODM Raila Odinga waziri wa usalama wa ndani Dr.Dred Matiang’I,gavana james ongwae,seneta sam ongeri,mwakilishi wa kina mama janet ong’era kati ya viongozi wengi kutoka sehemu zote za nchi.
Akizungumza katika kongamano hilo gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae aliwaomba wote washirikiane na Rais na kinara wa ODM kufanikisha mahitaji na mapendekezo yalioratibiwa kwa ripoti ya jopo la maridhiano maoni ambayo yaliungwa mkono na kinara wa ODM Raila Odinga ambaye alisema kuwa kuna uwiano na dhamira bora kwa yalio kwenye BBI.
Siku iyo hiyo haikukosa sarakasi pale ambapo magari anayofaa kutumia naibu gavana wa Kisii Joash Maangi yalipochukuliwa rasmi na walinda usalama kwa msingi kuwa yalikuwa yapelekwe kunagaliwa kule Kisumu ilivyo kawaida ambapo tuhuma zilisambaa kuwa upinzani wake dhidi ya BBI ndio uliomletea masahibu hayo.
Inafaa kukumbukwa kuwa naibu gavana huyu ni mwendani wa karibu wa naibu wa Rais William Ruto na amekuwa akimpigia debe sana naibu rais kuwa rais mwaka wa 2022 akifutilia mbali wale wanaompendekeza waziri wa usalama wa ndani Dr.Fred Matiang’i kuwania urais akidai kuwa Matiangi hajasema wala kuonyesha nia hiyo.
“Mimi sina shida na Matiangi walakini kuna mahasimu wangu wa kisiasa ambao wanataka kupenya kisiasa na kujificha chini ya matiangi’ kuuficha uovu ambao wako nao hasa ufisadi na hilo lazima mtoto wetu wa wakisii wote ajue”,alimaka maangi akiongeza kuwa kwa sasa anamuunga naibu wa rais mkono kuwa rais na kuwa matiangi ni mfanyikazi wa serikali , hajasema kuwa anataka kiti cha kisiasa na wakati atakaposema hana budi kumuunga mkono.