Sossion azidi kupinga uhamisho wa walimu.

1
7
Sossion
Katibu mkuu wa chama cha walimu KNUT Bwana Wilson Sossion. PICHA/HISANI

Chama cha walimu nchini KNUT kimesimama kidete kupinga hatua ya kuhamishwa kwa walimu kuelekea shule za mbali na nyumbani kwao.

Akizungumza pale Mombasa siku ya Jumanne katika kongamano la walimu wa shule za msingi, Katibu mkuu wa chama hicho bwana Wilson Sossion amedokeza kuwa walimu wengi ambao tayari wamehamishwa wanazidi kuteseka bila hata ya marupurupu ya kuwakimu.

Sossion ametishia kufutiliwa mbali kwa tume ya kuwaajiri walimu TSC akidai kuwa imekosa mwelekeo kamili.

1 COMMENT