Mwanaume amujeruhi mkewe kwa maji moto huko Gatundu.

2
104
Mwanaume
Maji moto PICHA/HISANI

Mwanaume mmoja mwenye umri wa makamo amemujeruhi bibi yake vibaya baada ya kumumwagia maji moto katika kijiji cha Kanjuku huko Gatundu Kasikazini.

Kulingana na Majirani, Samuel Nguta amekuwa na mzozo wa mda mrefu na Anne Njeri ambaye ni mkewe.

Duru za kuaminika zinasema kuwa Nguta aliteketeza nyumba kwa petroli kabla ya wasamaria wema kumwokoa mkewe.

Mke huyo kwa sasa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Igegania level 4. 

Joshua Kung’u mambaye ni chifu wa eneo hilo amelaani kitendo hicho huku akiziomba familia kutatua mizozo kati yao kwa njia ya kisheria.

Mwanaume huyo anaendelea kusakwa na polisi baada ya kuponyoka hamaki ya wanakijiji.

2 COMMENTS